Home Habari za michezo MAMBO NI MOTO PRISONS SIO POA………UNAAMBIWA KUIFUNGA SIMBA, YANGA MILIONI 10 MEZANI

MAMBO NI MOTO PRISONS SIO POA………UNAAMBIWA KUIFUNGA SIMBA, YANGA MILIONI 10 MEZANI

Sasa washindwe wao. Ndivyo unaweza kusema kufuatia udhamini walioupata Tanzania Prisons kutoka kampuni ya mbolea ya ruzuku, Bens Agro Star wenye thamani ya Sh150 milioni ukiambatana na bonasi kadhaa.

Udhamini huo utakuwa wa msimu mmoja ambapo kampuni hiyo itatoa kiasi hicho huku ikiahidi ofa kwa wachezaji na benchi la ufundi ikiwa ni kuhakikisha inafanya vizuri.

Akizungumza baada ya kusaini na kukabidhiana mkataba huo ambao umefanyika jijini hapa, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Patrick Mwalunenge amesema mbali na kutoa fedha hizo lakini kutakuwapo ofa mbalimbali.

Bonasi hizo ni pamoja na Sh10 milioni iwapo Prisons itazifunga Yanga na Simba, lakini kutoa Sh1 milioni kwa kila bao kwenye ushindi huku kocha mkuu akilamba Sh 500,000 na mwisho wa msimu atatafutwa mchezaji bora atakayejengewa nyumba.

“Kuhusu suala la usafiri wa basi la kisasa tutalifanyia kazi huko mbeleni, pamoja na kukarabati hostel za wachezaji, hivyo nimuombe kocha Fredi Felix ‘Minziro’ kukaza sana pamoja na wachezaji wake”

“Hatujapotea njia kuweka Udhamini hii ni timu hii kubwa yenye historia kubwa hivyo katika mkataba huu kuna kipengele cha kuongeza kandarasi” amesema Mwalunenge.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ajabu Kifukwe amesema udhamini huo utakuwa chachu kubwa katika kuhamasisha matokeo mazuri na tutawatangaza katika timu zote nne ikiwamo ya wanawake na vijana.

Mtendaji Mkuu wa Tanzania Prisosns, Ajabu Kifukwe akitoa taarifa fupi kabla ya utambulisho rasmi wa mdhamini mkuu wa klabu hiyo msimu wa 2023/24

“Tunaahidi kushirikiana vizuri na wadhamini wetu na tutawatangaza popote timu itakapokuwa, tunaamni tutafanya makubwa katika ligi zetu” amesema Kifukwe

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amesema udhamini huo utakuwa chachu katika kuendeleza michezo jijini Mbeya akiomba wadau wengine kujitokeza.

“Hivyo niwaombe Prisons msiishi kijeshi licha ya timu kuwa ya Jeshi, tunahitaji kuona mkishiriki shughuli za kijamii na kuwa karibu zaidi na wananchi ili wajue ni timu yao,” amesema Malisa aliyewamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.

SOMA NA HII  MAXI NZEGELI AZUA HOFU.... CHAMA, ONANA WAPEWA KAZI MAALUM