Home kimataifa ARSENAL KUMTOA LACAZETTE

ARSENAL KUMTOA LACAZETTE


 MABOSI wa Arsenal inaonekana kabisa hawana mpango na nyota wao Alexandre Lacazette na wanataka kumfanyia mabadilishano na mchezaji kutoka Sevilla, Youssef En-Nesyri.

Arsenal hesabu zao ni kuweza kuona kwamba wanampata staa huyo kwenye usajili wa Januari mwakani kwa kuwa wanaamini kwamba wakimpata huyo basi watapata ubingwa wa Ligi Kuu England, msimu ujao.

Mikel Arteta ambaye ni Kocha Mkuu wa Arsenal hana mpango na mshambuliaji wake Lacazette hivyo anaamini kwamba anaweza kutumika katika ishu ya kumpata mshambuliaji kutoka Sevilla.

Mkataba wa nyota huyo unameguka mwishoni mwa msimu huu na kwa jinsi picha inavyoonekana hataongezewa kandarasi nyingine hivyo wanataka kuhakikisha kwamba anasepa hapo Januari kukwepa suala la Lacazette kuondoka bure.

Licha ya kuwa hivyo inatajwa kuwa mashabiki wa Arsenal hawaelewi juu ya mpango huo na wanahitaji kumuona nyota huyo anaendelea kuwa mali yao kwa kuwa ni moja ya kipenzi cha mashabiki.

SOMA NA HII  WAKATI JAHAZI LA MAN UTD LIKIWA HALIELEWEKI...RIO FERDINAND ATABIRI HAYA KUHUSU RONALDO...