Home news YANGA WALIA NA SIMBA KISA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO

YANGA WALIA NA SIMBA KISA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO


 NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa nguvu za wachezaji wengi zilitumika kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba jambo ambalo limewafanya wacheze chini ya kiwango mbele ya Kagera Sugar.

Yanga iliendelea pale ilipoishia msimu wa 2020/21 ilipotua Uwanja wa Kaitaba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa ilishinda bao 1-0 na lilipachikwa na Tonombe Mukoko aliyefanya timu hiyo kusepa na pointi tatu.

Iliporudi tena Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-1 Yanga mtupiaji alikuwa ni kiungo Feisal Salum ambaye alionyesha ubora kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.


Nabi amesema:”Ninafurahi kuona tumeshinda na kupata pointi tatu, lakini ukweli ni kwamba wachezaji wamejitahidi kwani nguvu kubwa walitumia kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Simba na niliwaambia kwamba wanapaswa wapambane kupata ushindi,” .


Kituo kinachofuata kwa Yanga ni Uwanja wa Mkapa ambapo leo watakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Geita Gold ambayo imetoka kunyooshwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC.

Nabi amebainisha kuwa anahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo kwa kuwa ni muhimu kwao kupata pointi tatu ili waweze kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

SOMA NA HII  KUMBE!MANARA NA MORRISON WALIKIAMSHA TENA KISA MO