Home news NAMNA SIMBA WALIVYOPAMBANIA POINTI TATU DODOMA

NAMNA SIMBA WALIVYOPAMBANIA POINTI TATU DODOMA


 MIKIKIMIKI ya mchezo wa Ligi Kuu Bara imeendelea kwa mara nyingine tena Simba ya Didier Gomes iliibuka na ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri Dodoma baada ya ubao wa Uwanja wa Jamhuri kusoma Dodoma Jiji 0-1 Simba. 


Kagere jana Oktoba Mosi alifunga bao hilo akitumia pasi ya Chris Mugalu aliyetoa pasi akiwa nje ya 18 na Kagere alipachika bao hilo kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 likamshinda mlinda mlango Hussein Masalanga.

Katika mchezo wa jana, Gomes hakuwa na namna kwa kuwa alifanya mabadiliko ya lazima mara tatu baada ya nyota Sakho kutoka nafasi yake ikachukuliwa na Rarry Bwalya,  beki Kenedy Juma naye alitoka nafasi yake ikachukuliwa na Inonga hiyo ilikiwa ni kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili mchezaji wao wa tatu pia aliumia ambaye ni Taddeo Lwanga baada ya kuchezewa faulo na Salmin Hoza ambaye alionyeshwa kadi ya njano.

Dodoma Jiji inayonolewa  na Kocha Mkuu, Mbwana Makata ilikamilisha dakika 90 ikiwa pungufu baada ya nyota wao Anuary Jabir kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 44 kwa kumchezea faulo Kenedy Juma. 

Jitihada za Simba kusaka ushindi zilijibu kipindi cha pili baada ya Gomes kuwatumia nyota wake wote wa kazi katika safu ya ushambuliaji ikiwa ni pamoja na John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu. 
Washambuliaji hao walikuwa na moto msimu uliopita ambapo Mugalu alifunga mabao 15, Kagere alitupia mabao 13 na Bocco mabao 16.

Dodoma Jiji walikwama kutumia nafasi ambazo walizitengeneza kupitia kwa Cleophance Mkandala pamoja na Seif Karihe ambao walikuwa ni mwiba kwa mchezo wa jana.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza Simba kushinda msimu wa 2021/22 baada ya ule wa awali kupoteza pointi mbili walipoteza pointi mbili mbele ya Biashara United. Leo kikosi cha Simba kimerejea Dar baada ya kusepa na pointi tatu kutoka Dodoma Jiji.


SOMA NA HII  WAKATI SIMBA IKIZIDI KUVUNJA REKODI ZA AL AHLY CAF...BARBARA KUMBE ALISHALIONA HILO MAPEMA...