Home Simba SC HAWA WANNE HAWATAKUWA SEHEMU YA SIMBA MSIMU UJAO, WAWILI WA KIMATAIFA

HAWA WANNE HAWATAKUWA SEHEMU YA SIMBA MSIMU UJAO, WAWILI WA KIMATAIFA

 


IMEELEZWA kuwa miongoni mwa wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara msimu ujao ni pamoja na mshambuliaji wao wa kimataifa Junior Lokosa.

Lokosa ni ingizo jipya ambaye alisajiliwa kwa sababu za mashindano ya kimataifa ambayo Simba inashiriki ikiwa imeweza kutinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Raia huyo wa Nigeria ambaye usajili wake ulikamilika na hati ya utambulisho ilikuwa mikononi mwa Simba kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Kaizer Chief.

Ila baada ya usajili wake hajacheza mechi hata moja kwenye ligi ya mabingwa Afrika kwa kile ambacho Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes alieleza kuwa hayupo fiti na badala yake alipewa program maalumu ili arejee kwenye ubora wake.

Kwenye msafara ambao upo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa kesho Aprili 9 dhidi ya Al Ahly jina lake halipo. Habari zinaeleza kuwa tayari ameshapigwa chini mazima na amerejea nchini Nigeria kusaka mishe nyingine.

Mwingine ambaye amewekwa kwenye orodha hiyo ni beki Peter Mudhuwa raia wa Zimbabwe ambaye alisajiliwa kwa mkopo kutoka Klabu ya Highlanders FC.

Beki huyo naye maisha yake ndani ya Simba yamekuwa na drama nyingi akiwa hajacheza mchezo hata mmoja wa Ligi ya Mabingwa kama mshikaji wake Junior.

Pia mzawa Gadiel Michael ambaye ni beki pia yeye inaelezwa kuwa ameomba kusepa ndani ya kikosi hicho kutokana na kukosa namba kikosi cha kwanza kwa kuwa mfalme wa namba yake ni Mohamed Hussein.

Yeye anatajwa kuomba kusepa na mshikaji wake Ibrahim Ajibu ambaye wote walikuwa pamoja Yanga na waliibuka pamoja Simba.

Hivi karibuni Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliweka wazi kuwa kuhusu Lokosa hawatazungumzia suala hilo mpaka wamalize mechi zao za kimataifa.


SOMA NA HII  ISHU YA MIQUISSONE KURUDI TENA SIMBA...TRY AGAIN APIGILIA MSUMARI WA MOTO...