Home Ligi Kuu KOCHA MTIBWA SUGAR BADO HAJAFIKIRIA KURUDI BONGO

KOCHA MTIBWA SUGAR BADO HAJAFIKIRIA KURUDI BONGO


  
KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery ameikacha Mtibwa Sugar kwa kuwa bado hajapanga ratiba ya kurudi Bongo kwa sasa licha ya ratiba kuwekwa wazi.


Hitimana kwa sasa yupo Rwanda ambapo alirudi kwa ajili ya mapumziko yaliyotokana na kusimamishwa kwa ligi baada ya siku 21 za maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Thiery amesema kuwa bado yupo Rwanda kwa sasa na hajafikiria kuhusu kurudi Tanzania.

“Kwa sasa sijafikiria kurudi Tanzania kwa kuwa kuna vitu ambavyo ninakamilisha, ila sidhani kama itakuwa ni kwa muda huu,” amesema Thiery.

Thiery amewahi kuifundisha Biashara United ya Mara kisha akafukuzwa na kuibuka ndani ya Namungo FC ya Ruangwa ambayo aliipandisha kutoka Ligi Daraja la Kwanza mapa ndani ya Ligi Kuu Bara napo alichimbishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa matokeo mabovu.

Licha ya kupigwa chini ndani ya Namungo FC aliweza kukifanikisha kikosi hicho kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 jambo lililokipa nafasi kikosi hicho kuwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho kwa sababu Simba inawakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza jumla ya mechi 22.

Kesho Ijumaa, Aprili 9 ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Azam FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI