Home Yanga SC FEI TOTO KUWEKWA RADA ZA TP MAZEMBE, DILI LA MUKOKO IPO HIVI

FEI TOTO KUWEKWA RADA ZA TP MAZEMBE, DILI LA MUKOKO IPO HIVI

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hauna tatizo ikiwa itatokea timu inahitaji mchezaji wake ili ipate huduma yake kwa kuwa mpira ni biashara.

Hivi karibuni imekuwa ikielezwa kuwa kiungo wao Mukoko Tonombe anahitajika na Kaizer Chief pia nyota wao Feisal Salum alikuwa anatajwa kuingia rada za TP Mazembe.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hakuna jambo ambalo linashindikana kwenye ulimwengu wa mpira hasa unapozungumzia biashara ya wachezaji.

“Taarifa nyingi zimekuwa zikieleza kwamba kuna wachezaji ambao wanahitajika ndani ya kikosi cha Yanga na timu nyingine ikiwa ni Kaizer Chiefs, TP Mazembe hakuna ubaya.

“Ikiwa wachezaji wako wanatajwa sehemu moja tofauti maana yake ni kwamba wanafuatiliwa hata sisi pia huwa tunafuatilia wachezaji wa timu nyingine ili tuweze kuwasajili.

“Hivyo kama TP Mazembe ama Kaizer Chief wanahitaji wachezaji kutoka Yanga ni suala la kukaa chini na kuzungumza kila kitu kinawezekana,” alisema.

Tonombe ambaye ni ingizo jipya kutoka AS Vita ya Congo amesema kuwa naye amekuwa akiskia taarifa kwamba kuna timu zinamuhitaji ila yeye kwa sasa ni mchezaji wa Yanga.

SOMA NA HII  KIVULI CHA MAYELE KINAVYOMTESA GUEDE YANGA...MUSONDA AMESHINDWA....?