Home Uncategorized KISA BEKI, MABOSI SIMBA WAISHINDWA YANGA

KISA BEKI, MABOSI SIMBA WAISHINDWA YANGA


MABOSI wapya wa Yanga wamefanikisha mipango ya kumuongezea mkataba wa miaka mitatu beki wake, Gadiel
Michael ambaye ilikuwa kiduchu tu asaini Simba.

Dau alilowekewa mezani beki huyo lilikuwa ni Shilingi Milioni 40 na mshahara wa Milioni tatu. 

Habari za uhakika zinasema kuwa ni kwamba beki huyo wamefikia makubaliano na viongozi wa timu hiyo na wamemhakikishia mambo mazuri yanakuja akae mkao wa kula.

Mmoja wa viongozi wa Yanga, Fredrick Mwakalebela licha ya kutoweka wazi lakini alisisitiza kwamba kila kitu freshi Wanayanga watulie wanasuka chama la maana.

Gadiel ni miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo waliofanya vizuri na Yanga msimu uliopita. Habari zinasema kwamba Simba walishamseti lakini akawaambia ataendelea kubaki Yanga

SOMA NA HII  VIINGILIO VYA IHEFU vs YANGA HIVI HAPA