Home Habari za michezo KUHUSU UDHAMINI WA CRDB ….BARBARA ATUPA KIJEMBE YANGA…AFUNGUKA KUHUSU RANGI ZA KIJANI...

KUHUSU UDHAMINI WA CRDB ….BARBARA ATUPA KIJEMBE YANGA…AFUNGUKA KUHUSU RANGI ZA KIJANI KWENYE JEZI YA SIMBA..


Klabu ya Simba imebustiwa na benki ya CRDB baada kupewa hundi ya Sh25 milioni kwa ajili ya Tamasha la Simba Day.

Hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo imefanyika katika Makao makuu ya CRDB ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji mkuu wa CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Nsekela amesema wameona fursa kwao kusapoti Simba kwenye Tamasha lao la Simba Day.

Nsekela amesema wao kama benki ya CRDB imekuwa ikijihusisha na michezo na lengo kuinua vipaji.

“Tupo kwenye basketball na tumeiinua kwa kiwango kikubwa mchezo huu na kwa wale wachezaji ambao wanafanya vizuri tunawasapoti upande wa kuwasomesha kwenye elimu ya viwango vya juu,amesema Nsekela na kuongeza;

“Tumeona  tuipe udhamini Simba ili kamati ya maandalizi ifanye vitu vizuri kwenye tukio hilo kubwa”.

Upande wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema Simba Day inazidi kuwa bora zaidi tofauti na miaka ya nyuma.

Barbara amesema CRDB ni benki kubwa na imeenda kuwasapoti na jambo kubwa kwao kufanya kazi na kampuni ambayo wanaendana nayo.

“Huu ni mwanzo na huko mbele ningetamani kuiona CRDB kwenye jezi, kwenye tamasha letu kutakuwa na viburudisho kuanzia mwanzoni mpaka mwisho, amesema Barbara na kuongeza;

“Nakaribisha hata kampuni zisizokuwa na rangi nyekundu zifanye kazi pamoja na sisi na ndio maana hata CRDB wana rangi rangi ya kijani lakini hatujabadilisha nina heshimu”

Mkataba huo unakuja ikiwa zimepita siku mbili tangu Simba itangaze mkataba na mdhamini mkuu wa timu hiyo M-Bet wenye thamani ya Sh26.1 bilioni.

SOMA NA HII  HUKU SIMBA NA YANGA ZIKIJIVUTA VUTA...AZAM FC WAPIGA HATUA MOJA MBELE KWENYE HILI...