Home Azam FC HUKU SIMBA NA YANGA ZIKIJIVUTA VUTA…AZAM FC WAPIGA HATUA MOJA MBELE KWENYE...

HUKU SIMBA NA YANGA ZIKIJIVUTA VUTA…AZAM FC WAPIGA HATUA MOJA MBELE KWENYE HILI…

Habari za Michezo leo

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wanatarajia kuweka kambi ya majuma mawili visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Ofisa Habari wa timu hiyo, Thabit Zacharia ‘Zaka Zakazi’, amesema kambi hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya kulisaidia benchi lao la ufundi kujenga muunganiko mzuri kwa wachezaji wao, ambao wametawanyika baada ya mapumziko mafupi waliyopewa tangu walipotolewa Kombe la Mapinduzi.

“Tutaingia kambini Januari 23 tukianzia Azam Complex kwa siku mbili kisha tutakwenda Zanzibar kumalizia maandalizi hayo na baada ya hapo tutakuwa tayari kwa mechi za Ligi Kuu na mashindano mengine,” amesema Zaka Zakazi.

Ofisa huyo wa kitengo cha habari, amesema wameichagua Zanzibar kwa sababu ni sehemu tulivu na rafiki kupata miundombinu ikiwemo viwanja vizuri vitakavyoliwezesha benchi lao la ufundi kupanga mikakati yao kwa ubora.

Amesema pamoja na mazingira mazuri na utulivu wa Zanzibar lakini kitu kingine kinachowafanya kuweka kambi visiwani humo ni uharaka wa kupata mechi za kirafiki.

SOMA NA HII  KUHUSU WACHEZAJI SIMBA KUDAI DAI POSHO ZAO..... UONGOZI WAFUNGUKA HAYA