Home Habari za michezo KUHUSU WACHEZAJI SIMBA KUDAI DAI POSHO ZAO….. UONGOZI WAFUNGUKA HAYA

KUHUSU WACHEZAJI SIMBA KUDAI DAI POSHO ZAO….. UONGOZI WAFUNGUKA HAYA

Habari za Simba SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema hakuna mchezi yeyote wa Simba ambaye anadai posho yake.

Try Again ameyasema hayo mara baada ya kuwepo kwa madai kuwa mpasuko ndani ya Simba umesababishwa na baadhi ya wachezaji kutolipwa posho zao.

“Hakuna mchezaji hata mmoja ambaye hajalipwa posho zake, huu ni uzushi ambao hauna maana yoyote. Ni maneno ya wapinzani, ni maneno ya kupuuzwa,” alisema Try Again.

Try Again aliongeza kuwa, Simba ndio timu pekee ambayo inatoa bonus kubwa kwa wachezaji katika mechi na zote zinalipwa kulingana na matakwa waliyojiwekea.

“Mechi ya Al Ahly ya hapa, tuliwaahidi wachezaji wakishinda tutawapa Mil. 500 lakini hawakushinda, mechi ya marudiano tuliwaahidi kuwapa Bilioni moja lakini nayo hawakushinda,” aliongeza Try Again.

SOMA NA HII  KIPA MBRAZILI KATEMA BUNGO BWANA, AMESHAPEWA MKONO WA KWAHERI, MWAMBA HUYU HAPA SASA KUTOKA AMERIKA ATUA MSIMBAZI