Home kimataifa HWANG HEE-CHAN ACHEKEKEA KUPACHEKA NA NYAVU PREMIER LEAGUE

HWANG HEE-CHAN ACHEKEKEA KUPACHEKA NA NYAVU PREMIER LEAGUE

 NYOTA mpya wa Wolves Hwang Hee-chan ambaye yupo hapo kwa mkopo baada ya kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England akitokea Klabu ya Leipzig amesema kuwa ni furaha kwake kuingia katika orodha ya watupiaji ndani ya kikosi hicho.

Alitupia kwa mara ya kwanza akiwa na Wolves,  Septemba 11 katika mchezo wa Ligi Kuu England na ubao wa Uwanja wa Vicarage Road ulisoma Watford 0-2 Wolves. 

Ilikuwa dakika ya 74 Francisco Sierralta alijifunga na ninja Hwang Hee-chan alipachika bao la pili dakika ya 83 na anakuwa ni mchezaji wa kwanza ndani ya Wolves kupachika bao kwa msimu wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu England. 

“Ni heshima kwangu kufunga bak katika majukumu yangu hasahasa katika Premier League.  Ilikuwa ni ndoto yangu kuja hapa tangu nikiwa mdogo. Nina furaha kubwa sana na kiukweli ninawakubali watu ambao wamenisaidia mimi kufika hapa ikiwa ni lamoja na familia,”.

Leo Wolves ina kazi ya kufanya mbele ya Tottenham Hotspur kusaka ushindi katika mchezo wa Carabao utakaopigwa Uwanja wa Molineux.

SOMA NA HII  WISSA MTIBUAJI WA MAMBO ULAYA