Home Habari za michezo KUHUSU KUPATA NAFASI YA ‘KUSHINE’ NA YANGA ….OKRAH KAGUNA KISHA KAKASEMA HILI….

KUHUSU KUPATA NAFASI YA ‘KUSHINE’ NA YANGA ….OKRAH KAGUNA KISHA KAKASEMA HILI….

Habari za Yanga leo

Yanga inaendelea kujifua kambini Avic Town Kigamboni ikijiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho (ASFC) zitakazopigwa mwezi ujao mara baada ya fainali za Afcon 2023, huku nyota mpya wa timu hiyo, Augustine Okrah akiwatoa hofu mashabiki akiwaambia watulie.

Okrah aliyewahi kuwika na Simba msimu uliopita, amesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo akitokea Bechem ya Ghana na alicheza kwa dakika chache mechi ya Kombe la Mapinduzi 2024 kabla ya kutolewa uwanjani baada ya kuumia na sasa amefunguka anaendelea vyema na amejipanga kuwapa raha mashabiki.

Nyota huyo Mghana ni kati ya nyota wapya watatu waliosajiliwa dirisha hili na Yanga akiwamo Joseph Guede raia wa Ivory Coast na Shekhan Ibrahim Khamis aliyekuwa JKU ya Zanzibar wakichukua nafasi za Jesus Moloko, Hafiz Konkoni na Crispin Ngushi.

Okrah alisema anatambua uwepo wa wachezaji bora katika maeneo anayocheza, lakini amejipanga vyema na ana uhakika atapenya kwenye kikosi cha kwanza na kuwapa furaha mashabiki.

Staa huyo anayemudu kucheza winga zote mbili, sambamba na kiungo mshambuliaji (namba 10), anaamini atapata nafasi kikosini Yanga ambapo nafasi hizo wamekuwa wakicheza kwa ubora Maxi Nzengeli, Stephane Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Farid Mussa, Denis Nkane, Kennedy Musonda na Jesus Moloko alifungashiwa virago.

“Natambua ubora wa kila mchezaji wa Yanga hususan maeneo ninayocheza, hilo linanifanya kuungana nao na kufanya vyema kwa ajili ya manufaa ya timu pia inanipa ari ya kupambana zaidi ili kupata nafasi kikosini.

“Mimi sio mgeni hapa Tanzania, nimewahi kucheza Simba na sasa nimerudi nikiwa na Yanga nadhani tutakuwa na safu bora zaidi ya ushambuliaji na wapinzani wanapaswa kujipanga zaidi kutukabili.”

Okrah aliyeichezea Simba msimu uliopita kabla ya kuachwa na kurejea kwao katika timu ya Bechem United ambapo hadi anajiunga na Yanga alikuwa ameifungia mabao tisa na kutoa pasi za mabao mawili katika mechi 16.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi akimzunguzia Okrah, alisema ni mchezaji mzuri na kama atafanya vyema mazoezini basi atampa nafasi.

“Nimemuona ni mchezaji mzuri, kama ilivyo kawaida, natoa nafasi kwa mchezaji anayefanya vizuri mazoezini kwani tunachokifanya kwenye uwanja wa mazoezi ndicho tunafanya kwenye mechi, hivyo kila mtu ndani ya timu yetu ana nafasi kikosini,” alisema Gamondi.

SOMA NA HII  MAN UNITED KUVUNJA REKODI YAO YA USAJILI KWA RICE...MOYES AWAVIMBIA ...ATAKA MPUNGA MREFU ZAIDI...