Home Habari za michezo USIKU WA BALLON d’Or …,KATI YA HAWA NANI KUIBUKA MBABE….?

USIKU WA BALLON d’Or …,KATI YA HAWA NANI KUIBUKA MBABE….?

Habari za Michezo

Usiku leo Jumatatu 17/10 ndio usiku wa kufahamika mchezaji gani anakwenda kuondoka na ballon dior ikiwa kila mchezaji kutoka timu tofauti aliyebahatika kuwania kombe hilo anarekodi zake,

wajue baadhi ya mastaa, walio kwenye orodha ya kinyanga’anyilo hichi, wasifu wao, baadhi ya rekodi zao, pamoja na timu wanazotoka.

1. Karim Benzema
stika wa timu ya real madrid pia anaitumikia timu ya taifa ya Ufaransa, umri wa miaka 34. Benzema ndiye mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kushinda Ligi ya Mabingwa mara tano. Katika maisha yake ya klabu, ameshinda La Liga na Ligue 1 mara nne

Alishinda Ligi ya Mataifa ya UEFA 2020-21 akiwa na Ufaransa na anatarajiwa kuwa mchezaji mkubwa kwa nchi yake katika Kombe la Dunia la FIFA la 2022.

2. Robert Lewandowski
Stika mwenye umri wa 34 kutoka Brcelona pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya poland, Mshambuliaji huyu wa Poland alishinda mataji 8 ya Bundesliga na moja la Ligi ya Mabingwa, akifunga mabao 344 katika michezo 374.

Mwaka 2020 alikaribia zaidi jukwaa la Ballon d’Or alipofunga mabao 55 katika mechi 48 za kampeni hiyo, lakini akashindwa na Lionel Messi.

3. Erling Haaland
Strika mwenye umri wa miaka 22 kutoka timu ya taifa ya Norway anayekipiga katika timu ya machester city akitokea Borrusia Dortmund.

msimu wa 2019-20 akiwa na Salzburg, alikua kijana wa kwanza kufunga katika mechi tano mfululizo za UEFA Champions League. Alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu uliofuata. Mnamo 2020, Haaland alishinda tuzo ya Golden Boy, wakati 2021 alitawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Bundesliga.

Katika Premier League akiichezea Manchester City, amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi kufunga hat-trick tatu mfululizo katika michezo ya nyumbani.

4. Kylian Mbape.
Ni Mchezaji kandanda wa Ufaransa ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Ligue 1 ya Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, amekuwa mfungaji bora wa ligi kuu katika karne ya 21. Sasa amefunga mabao 139 (16 akiwa na ASM na 123 akiwa na PSG) kwenye Ligue 1 Uber Eats, mbele ya mchezaji wa zamani wa Paris Edinson Cavani na mabao yake 138.

Mbali na hao wengine ambao wapo kwenye kinyang’anyilo hichi ni Mohamed Salah, kutoka Liverpool, Cristiano Ronald (Machester United), Thomas Muller (Bayer Munich).

Uzuri ni kwamba kupitia Kampuni bora ya Tanzania, inakupa nafasi ya kuweka bashiri katika ushindani huu, pamoja na michezo kitaifa na kimataifa, mbali na hapa sokabet inakupa nafasi ya kucheza michezo ya Casino, slots na virtual games.

Tumia Sokabet the best Sports betting in Tanzania kuweka bashiri zako ili kunufaika na ushindi wenye bonusi lukuki.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA 'CHAMA' LAO HATARINI KUPOTEA LIGI KUU...MABOSI MTIBWA SUGAR WAIBUKA NA HILI JIPYA....