Home Azam FC KUHUSU YALE MADAI YA AZAM KUWAWEKEA MADAWA WAARABU…UKWELI WOTE HUU HAPA…WALIANZIA UWANJA...

KUHUSU YALE MADAI YA AZAM KUWAWEKEA MADAWA WAARABU…UKWELI WOTE HUU HAPA…WALIANZIA UWANJA WA NDEGE…

Taarifa kutoka Klabu ya Soka ya Azam;

Tumesikitishwa sana na taarifa zinazoendelea kuenea kwenye mitandao mbalimbali ya ndani na nje ya Afrika, zikituhusisha sisi Azam FC na hujuma dhidi ya wapinzani wetu, Al Akhdar SC.

Tunapenda kukanusha vikali kuhusika na jambo lolote baya dhidi Al Akhdar SC, tukiamini kwamba chanzo cha tuhuma dhidi yetu ni dhamira mbaya na ovu iliyolenga kututoa mchezoni (mind games).

Yawezekana ni kweli kwamba Al Akhdar SC wamepatwa na changamoto za kiafya, jambo ambalo ni la kawaida kwa binadamu hasa anapobadili hali ya hewa…na tunawapa pole kwa hilo na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi ili wapate nafuu mapema.

Lakini changamoto za kiafya kwa wachezaji wa Al Akhdar SC zilianza tangu wakiwa kwenye ndege kutoka kwao Libya kuja Tanzania.

Walipofika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar Es Salaam, mchezaji wao mmoja alikuwa na hali mbaya kiafya na ikabidi achukuliwe na gari la wagonjwa kuwahishwa hospitali.

Kwa hiyo kutuhusisha sisi na changamoto zao za kiafya siyo jambo la kiungwana hata kidogo.

Sisi hatuhusiki na lolote kwa sababu hatukuwaandalia hoteli, hatuwaandalia chakula wala hatukuwa na ukaribu wowote nao, ambao ungeweza kumfanya mtu awe na shaka na sisi.

Baadhi ya mitandao imeenda mbali na kusema tuliwanyima uwanja wa mazoezi. Ukweli ni kwamba tuliwaruhusu kufanya mazoezi kwenye uwanja wetu, kwa siku mbili mfululizo, Oktoba 14 na Oktoba 15, na walifanya. Mpira ni mchezo wa kiungwana, na sisi tunaamini katika uungwana.

SOMA NA HII  ZA NDAI KABISA...KISA MSHERY..MTIBWA KUISHITAKI YANGA ...WALIA KUTOLIPWA HATA 'NDURURU' YA MAUZO...