Home Habari za michezo KOCHA MAKI AWAUMBUA WALIOKUWA WAKIMBEZA STRAIKA ‘MZUNGU’….AWATAKA WATULIE KAMA MAJI KWENYE NDOOO…

KOCHA MAKI AWAUMBUA WALIOKUWA WAKIMBEZA STRAIKA ‘MZUNGU’….AWATAKA WATULIE KAMA MAJI KWENYE NDOOO…


KOCHA wa Simba, Zoran Maki, amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na haraka na uwezo wa mshambuliaji wa timu hiyo, Dejan Georgejevic, kwani tayari ameshaanza kuwaonyesha ubora wake wa kufunga ndani ya timu hiyo.

Dejan ambaye ni ingizo jipya, tayari amefanikiwa kufungua akaunti ya mabao ndani ya Simba mara baada ya kufunga bao katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo Simba walicheza dhidi ya Kagera Sugar.

kocha Maki alisema kuwa kwa wale wote ambao walikuwa wanahoji ubora na uwezo wa Dejan wanatakiwa kutulia kwani tayari wamejionea uwezo wake na ni jambo la subira kwa mchezaji mpya katika timu yoyote kuanza kwa kufanya vizuri.

“Wanatakiwa kuangalia kuifutilia timu kwa ukaribu lakini kuhusu Dejan labda huko mbeleni ndio walitakiwa kuhoji kuhusu ubora wake na sio kwa sasa kwani ni mapema mno kwa mchezaji mpya ndani ya timu.

“Lakini pia watakuwa wamejionea uwezo wake wa kufunga kupitia mchezo dhidi ya Kagera, kila kitu kitakuwa sawa, sio pekee tu kuna wachezaji wengine wengi tunaamini watakuja kutusaidia sana huko mbeleni na sio mapema hii na huo ndio mpira,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  BABA MZAZI WA FEI TOTO AINGILIA SAKATA LA MTOTO WAKE KURUDISHWA YANGA...MSIMAMO WAKE HUU..