Home Habari za michezo WAKATI PICHA ZA MANZOKI AKIWA UWANJA WA NDEGE KWA SAFARI ZIKISAMBAA ….NABI...

WAKATI PICHA ZA MANZOKI AKIWA UWANJA WA NDEGE KWA SAFARI ZIKISAMBAA ….NABI AENDELEA KUSISITIZA JINA LAKE YANGA…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa hajawahi kumhitaji mshambuliaji wa Vipers SC ya nchini Uganda, Cesar Manzoki raia wa Congo DR.

Manzoki hivi karibuni alihusishwa kuhitajika na Yanga, licha ya kuwepo tetesi za nyota huyo kusaini mkataba wa awali Simba.

Mkongomani huyo anaushawishi uongozi wa klabu yake kumruhusu kujiunga na Simba katika msimu huu.

Nabi alisema kuwa hajawahi kumhitaji mshambuliaji huyo katika mipango yake ya usajili wa msimu huu.

Nabi alisema kuwa wachezaji wote ambao amewahitaji kwa kupeleka mapendekezo kwa Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, wamesajiliwa na wapo katika kambi.

Aliongeza kuwa anakubali kiwango cha mshambuliaji huyo ambacho amekionyesha akiwa na timu yake ya Vipers katika msimu uliopita lakini siyo hitaji lake.

“Ukweli ni kwamba sijawahi kumhitaji Manzoki na hakuwepo katika orodha ya wachezaji ambao mimi nimewapendekeza katika usajili wangu wa msimu huu.

“Kutokuwepo katika mipango yangu, hiyo haileti maana kuwa ni mchezaji mbaya, ni mzuri ninaheshimu kiwango chake.

“Kwani katika timu yangu, wapo washambuliaji wa aina ya Manzoki kama vile Mayele (Fiston) na Makambo (Heritier), hivyo sioni sababu ya kumsajili,” alisema Nab

SOMA NA HII  FISTON ADAIWA KUTELEKEZA FAMILIA YAKE, YAMFUATA BONGO