Home Uncategorized RASMI MUANGOLA WA YANGA KUIKOSA SIMBA NOVEMBA 7

RASMI MUANGOLA WA YANGA KUIKOSA SIMBA NOVEMBA 7

 


IMEELEZWA kuwa nyota namba moja ndani ya Yanga kwa uzalishaji wa mabao kwa wageni Carlos Carlinhos hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Simba, Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.


Raia huyo wa Angola ametengeneza jumla ya pasi mbili za mabao yaliyofungwa na Lamine Moro ambaye ni kinara wa mabao kwa mabeki ndani ya Bongo.


Aliumia akiwa mazoezini wakati timu yake ilipokuwa kambini kwa maandalizi ya mechi ya ligi dhidi ya Polisi Tanzania kwenye enka na mpaka sasa anaendelea kupambania afya yake irejee kwenye ubora.


Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Shecky Mgazija amesema kuwa hali ya nyota huyo imetengamaa ila itakuwa ngumu kwake kuanza kwenye kikosi kitakachomenyana na Simba.


“Carlinhos yupo vizuri na anaendelea salama lakini hataweza kuwa kwenye kikosi kitakachocheza na Simba kwa kuwa hajafanya mazoezi muda mrefu hivyo hayupo fiti,” amesema.


Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 9 kibindoni ina pointi 23 inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi zake ni 19 zote zimecheza mechi 9.


Chanzo:Championi

SOMA NA HII  ALIYENYOOSHWA NA MWAKINYO TINAMPAY KUKUTANA NA MUZIKI WA MFAUME

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here