Home Simba SC BAADA YA KUTEMANA NA SIMBA..MIRAJI ATHUMAN AANIKA TABIA ZA MORRISON HADHARANI..

BAADA YA KUTEMANA NA SIMBA..MIRAJI ATHUMAN AANIKA TABIA ZA MORRISON HADHARANI..


MSHAMBULIAJI Miraj Athuman ‘Sheva’ anajiandaa kuanza maisha mapya nje ya Simba baada ya kumalizana na KMC, lakini akamtaja winga mtukutu, Bernard Morrison akisema tofauti anavyoonekana jamaa nyuma ya pazia ni mtu poa sana.

Miraji tayari alishaondolewa kwenye mpango wa kocha wa Simba, Didier Gomes na yupo hatua za mwisho kumalizana na KMC, alisema kuna madini alipewa na Morrison yanayompa jeuri ya kupambana na maisha.

Alikiri ni kweli Morrison ana vituko sana, lakini anapokuwa anahitaji kufanya kitu cha kimaisha hana masihara na hapendi kupotezewa muda.

“Maisha ya Morrison nyuma ya pazia ni mtu anayependa maendeleo na hana uchoyo, akikuona unafiti kufanya kazi eneo fulani anakutia moyo na kukwambia uongeze bidii ili upate heshima,” alisema Miraji na kuongeza kuwa;

“Morrison hapendi kuchanganya mafaili, wakati wa kazi anapenda muongelee kazi, wakati wa utani mtataniana. Jamaa ana roho ya peke yake, tuliokaa naye tumemfaidi vizuri sana.”

“Aliniambia Miraji, una kipaji, kuondoka Simba isiwe mwisho wako.”

SOMA NA HII  MAROUF TCHAKEI KUTUA SIMBA DIRISHA KUBWA...? UKWELI UNAOFAA KUJUA HUU HAPA...