Home Simba SC SIMBA YAANZA SAFARI KUELEKEA MUSOMA KUIFUATA BIASHARA UNITED

SIMBA YAANZA SAFARI KUELEKEA MUSOMA KUIFUATA BIASHARA UNITED


KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, klabu ya Simba leo asubuhi kimeanza safari kutoka Jijini Mwanza kuelekea Musoma mkoani Mara kuwafuata Biashara United kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu utakaopigwa kesho Alhamisi.

Simba iliondoka na nyota wake wote isipokuwa Wachezaji; Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Ally salami, Kennedy Juma pamoja na Meneja wa kikosi, Abbas Ally ambao waliachwa nchini Congo.

Simba ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na pointi zao 39, walizokusanya katika michezo 17 waliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia safari yao, Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Biashara na wamejipanga kwa vita ya kusaka pointi tatu muhimu.

β€œKikosi cha mabingwa wa nchi leo asubuhi kimeanza safari kutoka jijini Mwanza kuelekea mkoani Mara kuifuata Biashara United kwa ajilli ya mchezo wetu wa ligi utakaopigwa kesho.

β€œTunajua hautakuwa mchezo rahisi lakini tumejipanga kwa vita ya kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu katika mchezo huo, kwani malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ulio mbele yetu ili kuzidi kuongeza pointi za kuelekea kileleni mwa msimamo wa ligi,” amesema Manara.

SOMA NA HII  VIWIKO NDANI YA UWANJA MUDA WAKE UMEISHA