Home Habari za michezo SIMBA BILA CHAMA SAWA NA ‘KIBOGOYO’ TU…KIBU DENIS AKAOMBEWE JAMANI…

SIMBA BILA CHAMA SAWA NA ‘KIBOGOYO’ TU…KIBU DENIS AKAOMBEWE JAMANI…

Ikicheza bila Clatous Chama Simba SC imeambulia pointi moja mbele ya Singida Big Stars ‘SBS’ mtanange uliofanyika jana jioni katika dimba la Liti Singida.

Chama amefungiwa michezo mitatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani katika mchezo wa Ligi Kuu.

Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kubaki katika nafasi ya 2 kwa kuwa na pointi 18 huku SBS ikisogea hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi kama hizo.

Simba iliuanza mchezo huo taratibu kwa kwa kushambulia kwa kushtukiza lakini mashambilizi yote yalikuwa yakiishia kwa kipa wa SBS Khomany Abubakary.

Dakika ya 8 ya mchezo Mzambia Patrick Phiri alishindwa kumalizia krosi ya Shomari Kapombe akiwa na kipa Khomeny Abubakary alipiga mpira uliotoka nje.

SBS ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa winga Deus Kaseke aliyemaliza krosi ya Said Ndemla.

Hadi mapumziko SBS walikuwa mbele kwa bao 1-0 ambapo kipindi Cha pili Simba walikianza kwa kufanya mabadiliko ya kumtoa Jonas Mkude na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Banda

Beki wa kati Abdulmajib Mangalo alikuwa nasiku nzuri kazini kwani aliweza kumkaba vilivyo Moses Phiri.

Akiwa na kipa Kibu alipoteza nafasi ya wazi dakika ya 48 mara baada ya kutengewa pasi na Pape Sacko lakini shuti lake lilipaa juu ya lango.

Dakika ya 58 Simba ilifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Banda mara baada ya kuwapiga chenga mabeki wa SBS na kisha kufunga.

Dakika ya 78 Mgunda alimtoa Kibu Denis na nafasi yake ilichukuliwa na Khabib Kyombo.

Mchezo huo ulihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walianza kuingia uwanjani saa tatu asubuhi.

Ilivyofika saa saba mchana tayari uwanja ulikuwa umejaa sehemu zote mzunguko na VIP.

SBS: Abubakary,Godfrey,Batambuzi,Mangalo,Biemes,Gomes,Dario,Kaseke,Ndemla Cruz,Kagere.Rodrigues

SIMBA: Beno,Kapombe,Tshabalala,Onyango,Inonga,Mkude,Kanoute ,Mzamiru,Kibu,Phiri Sacko.

SOMA NA HII  YANGA KUFANYIWA SAPRAIZI HII...HAIJAWAHI TOKEA BONGO...MABOSI WAPAGAWA