Home Habari za michezo BAADA YA KUFUNGWA JANA…TUMAINI LA SIMBA QUEENS LIMEBAKIA HAPA SASA…WAKIFELI NI NCHI...

BAADA YA KUFUNGWA JANA…TUMAINI LA SIMBA QUEENS LIMEBAKIA HAPA SASA…WAKIFELI NI NCHI IMEFELI…

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake, Simba Queens imeshindwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kufungwa bao 1-0 na mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns.

Mchezo huo wa nusu fainali uliopigwa katika Uwanja wa Prince Heritier Moulay El Hassan ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku ikiwachukua Mamelodi kujipatia bao lake dakika ya 76 kupitia kwa Boitumelo Joyce Rabele.

Simba Queens ambayo ilikuwa kundi A la mashindano hayo ilitinga hatua hiyo baada ya kushika nafasi ya pili na pointi sita nyuma ya wenyeji ASFAR ya Morocco iliyomaliza ikiwa ni kinara na pointi zake tisa.

Queens ilianza makundi kwa kufungwa bao 1-0 na ASFAR kisha kushinda michezo yote miwili ya mwisho kwa 2-0 dhidi ya Determine Girls na Green Buffaloes.

Katika mashindano ya msimu huu Queens ilikuwa na rekodi ya kipekee kwani ilikuwa timu ya pili kwenye historia kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi na kuifikia rekodi iliyowekwa na Malabo Queens ya Guinea ya Ikweta katika michuano hiyo mwaka jana.

Aidha Simba Queens ilikuwa ni timu ya kwanza kutoka Ukanda wa Cecafa kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo kwani kabla ya hapo hakuna timu yoyote iliyowahi kufika.

Kwa matokeo hayo Queens itashuka dimbani Jumamosi hii ya Novemba 12 katika Uwanja wa Stade Moulay Hassan kusaka mshindi wa tatu ambapo itacheza na timu itakayopoteza kati ya ASFAR na Bayelsa Queens ya nchini Nigeria.

SOMA NA HII  AFCON KULETA NEEMA HUU HAPA UWANJA MPYA UTAKAOJENGWA ARUSHA