Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUFANYA JAMBO LAO SASA NI ZAMU YA GEITA GOLD

BAADA YA YANGA KUFANYA JAMBO LAO SASA NI ZAMU YA GEITA GOLD

Geita Gold FC

Hatua hiyo inajiri baada ya Geita kuachana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’ baada ya mkataba wake kuisha tangu Mei 28 mwaka huu

UONGOZI wa Geita Gold uko kwenye mazungumzo na Kocha Mkuu wa KMKM, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho.

Hatua hiyo inajiri baada ya Geita kuachana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’ baada ya mkataba wake kuisha tangu Mei 28 mwaka huu.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo ililiambia Mwanaspoti, Morocco ndiye aliyependekezwa kuchukua nafasi ya Minziro kwa ajili ya msimu ujao.

“Seleman (Matola) alikuwa ni chaguo la kwanza ila baada ya kuona mambo hayaendi vizuri viongozi wakahamishia nguvu kwa Morocco ambaye hakutakuwa na shida kubwa sana kwenye kufikia muafaka suala la maslahi binafsi,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumzia hilo Mwenyekiti wa Geita, Leonard Bugomola alisema wapo makocha wengi waliotuma wasifu wao (CV) na mchakato wa kupitia jina moja baada ya lingine unaendelea ingawa suala la nani atachaguliwa hilo litafahamika hivi karibuni.
Kwa upande wa Morocco alipotafutwa na Mwanaspoti alisema yeye hajui lolote linaloendelea ingawa anasikia tu kuhusu jambo hilo.

“Nimesikia kama ambavyo nawewe umesikia ila siwezi kusema ni kweli au laah! muda utakapofika kila kitu nadhani kitakuwa wazi,” alisema.

Morocco ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ mbali na kuifundisha KMKM kwa sasa ila amewahi kuinoa pia Namungo.

SOMA NA HII  YANGA WAKOMAA NA PACHA WA NZEGELI.... ISHU IKO HIVI