Home news SAA KADHAA KABLA YA KUWAVAA WAMOROCCO…MKUDE NA KANOUTE ‘VIMEUMANA’…MATOLA AFUNGUKA A-Z…

SAA KADHAA KABLA YA KUWAVAA WAMOROCCO…MKUDE NA KANOUTE ‘VIMEUMANA’…MATOLA AFUNGUKA A-Z…


Wakati wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Mashindano ya Afrika Simba wakibakiza saa chache kushuka Uwanjani kupambana na wenyeji wao RS Berkane wekundu hao watawakosa viungo wao wawili muhimu.

Taarifa iliyotolewa na Simba inayoshiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kupitia kocha wao msaidizi Seleman Matola amesema Simba itaendelea kumkosa kiungo Jonas Mkude ambaye bado mgonjwa.

Mkude alikosa pia mchezo uliopita wa timu yake ikiwa ugenini dhidi ya US Gendarmerie ya Niger.

“Mkude bado hali yake haijakaa sawa mpaka sasa kwahiyo hakuna uwezekano wa kucheza mchezo huu,amesema Matola.

Mbali na Mkude vinara hao wa Kundi D pia watamkosa kiungo mwingine wa ukabaji Sadio Kanoute ambaye amepata maumivu katika mazoezi yao ya kwanza jijini Casablanca nchini Morocco.

” Kanoute aliumia tulipofika hapa Casablanca tulipokuwa tunafanya mazoezi ya kwanza pale na hali yake imeshindwa kukaa sawa mpaka sasa.

Simba itashuka Uwanja wa Manispaa ya Berkane kuumana na wenyeji wao Berkane inayoshika nafasi  ya tatu wekundu hao wakicheza mechi ya pili ugenini ambapo sasa watabakiza moja pekee.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 2 usiku kwa saa za Morocco huku Tanzania ikiwa saa 4 usiku.

SOMA NA HII  HAWA HAPA MASTAA 5 WA SIMBA SC WALIOKALIA KUTI KAVU...TARAJIA LOLOTE...