Home Habari za michezo BAADA YA UKIMYA MREFU….HATMA YA NKANE YANGA YATUPWA KWA NABI…ISHU NZIMA IKO...

BAADA YA UKIMYA MREFU….HATMA YA NKANE YANGA YATUPWA KWA NABI…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Yanga

Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga Denis Nkane tayari amerejea katika mazoezini ya kikosi cha klabu hiyo, baada ya kupona majeraha ya nyonga yaliyomuweka nje tangu mwishoni mwa mwezi Desemba, mwaka jana na sasa anamsikilizia kocha mkuu, Nassredine Nabi ampe nafasi kuanza kukiwasha.

Nkane alikaa nje kwa kipindi kisichopungua wiki sita akiuguza jeraha hilo la nyonga ambalo Daktari wa Yanga, Moses Etutu alithibitisha ilivunjika mfupa mdogo na kusababisha nyonga kujikunja lakini sasa yupo fiti na tayari kwa mapambano.

Akizungumza baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa za kikosi cha kwanza cha Yanga Nkane amesema “Niko poa sasa na siku yeyote mtaniona uwanjani nikicheza kwani nimepona tayari.”

Mbali na kiungo huyo, pia imethibitika kuwa Benard Morrison aliyekuwa nje tangu mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu akiuguza jeraha la nyonga, ameanza mazoezi mepesi, na wakati wowote ataungana na wachezaji wengine kwa mazoezi ya pamoja.

SOMA NA HII  KULEKEA MECHI YA JUMAPILI DHIDI YA USGN..PABLO AIBUKA NA HILI TENA...AJIPA JUKUMU KWA MASHABIKI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here