Home Simba SC UKIACHA, BANDA NA MHILU..HAWA HAPA WACHEZAJI WENGINE WAPYA WATANO WA SIMBA

UKIACHA, BANDA NA MHILU..HAWA HAPA WACHEZAJI WENGINE WAPYA WATANO WA SIMBA


BAADA ya mapumziko mafupi waliyopewa na benchi lao la ufundi, nyota wa Simba wakiwamo wale wapya waliosajiliwa hivi karibuni, wanatarajiwa kuliamsha dude upya  kabla ya kusafiri kwa ajili ya kambi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa inayoanza mwezi ujao.

Majembe mapya saba ambao watakutanishwa pamoja na wenzao waliokuwapo msimu uliopita ni winga kutoka Malawi, Peter Banda, kipa Jeremiah Kisubi, washambuliaji Yusuf Mhilu na Denis Kibu, mabeki Israel Mwenda na Henock Inonga Baka ‘Varane’ pamoja na winga Jimson Mwinuke.

SOMA PIAUKIACHA BANDA..HAWA HAPA NYOTA WENGINE AMBAO GOMES KAAGIZA WASAJILIE CHAP

Baadhi ya nyota hao wapya wameshatambulishwa rasmi na klabu hiyo ya Msimbazi, akiwamo Banda na Mhilu aliyewahi kukipiga Yanga, Ndanda na Kagera Sugar, huku wengine mpaka sasa ikifanywa siri wakisubiri siku ya kuwaachia mmoja mmoja na siku ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika jijini Dar.

Habari kutoka ndani ya Simba na kuthibitisha na baadhi ya wachezaji ni kwamba kuanzia jana {juzi} walitakiwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo, kisha leo {jana} kuingia kambini Mbweni ili kuanza maandalizi ya kwenda Morocco kuweka kambi baada ya ile ya Misri kushindikana.

Simba pia ilikuwa imepanga kama kambi ya Morocco ingekataliwa na Kocha Didier Gomes wangehamia Ufaransa, lakini Mfaransa huyo ameridhia kila kitu kifanyika Casablanca.

SOMA PIABAADA YA ‘KUFOKEWA’ NA MO DEWJI KISA KUMSIFIA MANARA, CHAMA AVUNJA UKIMYA…

“Tunaingia kambini  Jumatatu tayari kwa maandalizi ya msimu mpya, bahati nzuri mi sikusafiri kabisa, nilipumzika hapahapa Dar,” alisema mmoja ya wachezaji mahiri wa timu hiyo bila kutaka kuandikwa jina.

Kwa mujibu wa mmoja wa vigogo wa Simba ni kwamba timu yao itaondoka katikati ya wiki hii ili kuwahi kambi hiyo itakayoambatana na michezo ya kirafiki na kurejea siku chache kabla ya Simba Day.

Simba ndio mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo na Kombe la ASFC iliyotwaa mara mbili mfululizo na kwenye michuano ya kimataifa ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo msimu huu itashiriki tena sambamba na Yanga, huku Azam na Biashara United zitacheza Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  KISA SARE NA POWER DYNAMO JANA....MBRAZILI SIMBA APATA CHA KUJITETEA....