Home Uncategorized YANGA LEO TUNAMALIZANA MAHESABU MAPEMA KWA TOWNSHIP ROLLERS

YANGA LEO TUNAMALIZANA MAHESABU MAPEMA KWA TOWNSHIP ROLLERS


NOEL Mwandila, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi ya hatua ya kwanza ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana utakaopigwa lleo uwanja wa Taifa.

Mwandila amesema maandalizi ya wiki nne waliyofanya kuelekea msimu mpya wa ligi yametosha na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika uwanja wa nyumbani.


 “Maandalizi yamekamilika wachezaji wapo tayari kwa mchezo, tunahitaji kuhakikisha tunashinda nyumbani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri mechi ya marudiano ugenini,” amesema Mwandila.

Mlinda mlango Ramadhan Kabwili amesema kuwa wana imani ya kufanya vema hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  SIMBA YAFICHUA KINACHOWAPA NGUVU YA KUPAMBANA NDANI YA UWANJA