Home Azam FC AZAM FC WAMKANA SHABAN DJUMA….KUHUSU KUONEKANA MAZOEIZI UKWELI HUU HAPA…

AZAM FC WAMKANA SHABAN DJUMA….KUHUSU KUONEKANA MAZOEIZI UKWELI HUU HAPA…

Habari za Michezo

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Azam FC, Thabit Zakaria (Zaka Zakazi) ametoa ufafanuzi kuhusu picha zilizosambaa zikimuonyesha beki Djuma Shaaban akiwa pamoja na wachezaji wa timu hiyo wakifanya mazoezi.

Zaka amesema; “Ni kweli Djuma anafanya mazoezi na timu yetu kwa takribani wiki mbili sasa kwasababu aliomba kufanya mazoezi na sisi kwakuwa hakuwa na timu baada ya kuachana na Yanga hata hivyo Djuma ataendelea kufanya mazoezi na timu yetu hadi pale taarifa zaidi zitakapotolewa,”

Hata hivyo hapo awali taarifa zilisema Azam FC walimuhitaji beki huyo katika dirisha kubwa la usajili msimu huu lakini usajili huo uligonga mwamba baada ya golikipa Ally Ahmada kukataa kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa madai ya kuwa amechelewa kupewa taarifa na madirisha mengi ya usajili kwenye mataifa mengine yameshafungwa hivyo kuhofia kukosa timu

Kwakuwa Azam walikuwa tayari wameshafikisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kama inavyotaka kanuni za Ligi Kuu, walishindwa kumchukua Djuma kwa kuhofia kwenda kinyume na kanuni za ligi kwani angefanya idadi ya wachezaji 13.

Taarifa za kuaminika zinasema kuwa kocha wa Azam, Youssoupha Dabo bado anauhitaji na beki huyo na hivyo katika dirisha dogo la usajili ambalo hufunguliwa Desemba dili la beki huyo linaweza kukamilika.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA NA MSONGO WA KUKOSA MATOKEO MAZURI, WAISUSA SIMBA KWA MKAPA