Home news RUVU SHOOTING: HATUTAFANYA MAKOSA TENA MSIMU UJAO

RUVU SHOOTING: HATUTAFANYA MAKOSA TENA MSIMU UJAO


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umebainisha kwamba utasajili watu wa kazi kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ili kuepuka makosa ambayo waliyafanya msimu uliopita.

Msimu uliopita Ruvu Shooting ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 11 na pointi zake zilikuwa ni 41 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kuwa walipitia wakati mgumu msimu uliopita jambo ambalo linawafanya waongeze nguvu msimu ujao.

“Makosa ambayo tuliyafanya msimu uliopita hayo tumeyabaini na tunayafanyia kazi hivyo tutarejea tukiwa tupo imara zaidi.

“Mashabiki watupe sapoti na wawe na subira kwa kuwa ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa sawa na tutafanya usajili kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu,” alisema Bwire.

Ni nyota mmoja ambaye amesajiliwa na Ruvu Shooting kwa ajili ya msimu ujao ni Ally Mtoni, ‘Sonso’.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAKIRI KUZINGUA...WAOMBA MSAMAHA KWA STAILI HII MPYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here