Home Habari za michezo GAMONDI AWATULIZA MASHABIKI YANGA,…… UBINGWA UNABAKIA JANGWA MAMBO HADHARANI

GAMONDI AWATULIZA MASHABIKI YANGA,…… UBINGWA UNABAKIA JANGWA MAMBO HADHARANI

HUKU kikosi chake kikiendelea na maandalizi ya kabla ya msimu ‘pre season’ kwenye kambi yao ya AVIC Town Kigamboni, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewatuliza mashabiki wa Yanga kuwa kikosi chake kitatetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Yanga kwa msimu wa pili mfululizo ndiyo mabingwa watetezi wa mataji matatu makubwa ya mashindano ya ndani ambayo ni Ngao ya Jamiii, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Kombe la Ligi Kuu Bara.

Mataji hayo Yanga iliyatwaa katika kipindi cha misimu miwili ya utawala wa aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Mtunisia, Nasreddine Nabi ambaye alitangaza kutoendelea na Yanga mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.

Akizungumza kuhusiana na maendeleo ya kikosi chake, Gamondi aliliambia Championi Ijumaa: “Tumekuwa na wakati mzuri wa maandalizi ya kikosi chetu kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23 na baadhi ya michezo ya kirafiki ambayo tumefanikiwa kucheza imetupa mwanga wa wapi pa kuanzia.

“Tunafahamu utakuwa msimu mgumu kutokana na mabadiliko makubwa ambayo yamefanyika kwenye timu lakini niwahakikishie Wanayanga kuwa wana kikosi bora ambacho kitapambana kutetea mataji yote tunayoshilkilia na kwa umuhimu mkubwa ubingwa wa ligi.”

SOMA NA HII  YANGA YAPATA MAJANGA, LOMALISA OUT