Home Habari za michezo DAKTARI WA VIUNGO YANGA AKOMAA NA MAXI ISHU IKO HIVI

DAKTARI WA VIUNGO YANGA AKOMAA NA MAXI ISHU IKO HIVI

yanga leo

KATIKA kuhakikisha anakuwa bora na fiti zaidi, Kocha na Daktari wa Viungo wa Yanga, Mtunisia Youssef Ammar amepewa jukumu ya kumfanyisha programu ya binafsi kiungo mshambuliaji, Mkongomani Maxi Zengeli.

Mkongomani huyo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga katika kukiboresha kikosi hicho, ili kifanye vema katika msimu ujao ambao wanakwenda kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Yanga imemsajili kiungo huyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Meniema FC ya DR Congo ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Mghana, Bernard Morrison.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kiungo huyo mwenyewe amemuomba Youssef amsimamie programu hiyo ya mazoezi ya binafsi huko kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha anaongeza utimamu wa mwili.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kocha huyo amempa programu ya kuruka koni ambazo amezipanga uwanjani huku akikimbia mbio fupi kwa spidi sambamba na kukokota mpira.

Alisema kuwa mpira huo anaukokota huku akipita katikati ya koni akiwa anakimbia kwa spidi huku mara kadhaa kocha huyo akisikika akimwambia aongeze spidi zaidi.

Aliongeza kuwa programu hiyo anaifanya kabla ya kuanza mazoezi ya timu ya pamoja, lengo ni kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya Ngao ya Jamii.

“Maxi anaonekana amepania sana kuelekea msimu ujao na anaonekana anataka kuwa kuwa fiti kwa asilimia mia moja kabla ya Ngao ya Jamii, ili aonyeshe ubora wake kwa mashabiki.

“Juzi alionekana kufanyishwa mazoezi ya binafsi pekee chini ya kocha wa viungo Youssef, kabla ya mazoezi ya jioni ya pamoja na timu, juzi saa tisa alasiri alikuwa akifanya mazoezi ya utimamu ya mwili.

“Katika programu hiyo, kocha alimpangia koni akimtaka aziruke na wakati mwingine akikokota mpira akipita katikati ya hizo koni akiwa katika spidi kubwa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muargentina Miguel Gamondi alizungumzia hilo la kambi na kusema kuwa: “Kambi inaendelea vizuri na wachezaji wote wanajituma sambamba na kuonyesha uwezo ili wapate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

SOMA NA HII  MAUYA - ALICHOTUFANYIA SHOMARY KAPOMBE SIO KABISA