Home Habari za michezo BALEKE AANZA KUANDALIWA MAZINGIRA YA UFUNGAJI BORA, KRAMO ATAJWA

BALEKE AANZA KUANDALIWA MAZINGIRA YA UFUNGAJI BORA, KRAMO ATAJWA

Habari za Simba leo

KIUNGO mpya wa Simba, Aubin Kramo raia wa Ivory Coast, amesema malengo yake ni kuona timu inafanikiwa zaidi kuliko mafanikio binafsi, hivyo atahakikisha anawatengenezea nafasi za kufunga washambuliaji wa timu hiyo wakiongozwa na Jean Baleke.

Washambuliaji wengine ndani ya Simba wanaotarajiwa kuwepo ndani ya kikosi hicho ni nahodha John Bocco, Kibu Denis na Willy Onana.

Kramo ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao kwa ajili ya kuiboresha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, ambayo msimu ujao imepanga kufanya vema.

Kramo alisema kikubwa anataka kutimiza malengo ya timu yaliyopo kwa sasa ambayo ni kuchukua makombe yote watakayoshiriki katika msimu ujao.

Kramo alisema malengo hayo lazima yatimie msimu ujao, ili awape furaha na burudani mashabiki wa timu hiyo, kwa ushindi wa mabao mengi.

Alisema kuwa soka safi halitatosha kwake bila ya mafanikio ya ushindi, hivyo ni lazima atimize majukumu yake ya kutengeneza nafasi za kufunga mabao kwa washambuliaji na yeye mwenyewe kufunga akipata nafasi.

“Sitaangalia mafanikio yangu binafsi ndani ya Simba, hivyo nitakachokifanya ni kufanikisha malengo ya timu tuliyoyaweka katika msimu ujao.

“Mafanikio hayo ni kuchukua makombe yote tutakayoshindania, atakayefanikisha hayo ni sisi wachezaji, hivyo nitahakikisha ninawatengenezea washambuliaji nafasi za kufunga.

“Mafanikio ya timu ni yetu sote, hivyo akifunga mchezaji mwingine sio kitu kibaya, kwani ushindi utakaopatikana ni wa Wanasaimba wote,” alisema Kramo.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIKUBALI YAISHE KWA MAYELE.....KIFAA KIPYA KITAKACHOMRITHI HIKI HAPA...