Home Azam FC MAUYA – ALICHOTUFANYIA SHOMARY KAPOMBE SIO KABISA

MAUYA – ALICHOTUFANYIA SHOMARY KAPOMBE SIO KABISA


ALIYEIFUNGA Simba mechi ya dabi, Zawadi Mauya amefunguka namna beki Shomary Kapombe alivyotaka kuchomoa betri dakika za majeruhi alizokiri zilikuwa za kutumia akili kubwa, nguvu na ziliwatoa jasho kulinda bao lao.

Mauya alisema Kapombe aliwachachafya kipindi cha pili kwa kufika mara kwa mara langoni kwao akitokea pembeni, jambo lililowapa presha ya kuongeza umakini wa kulinda ushindi wao.

Alisema Kapombe ni beki aliye makini muda wote anaokuwa uwanjani na hakati tamaa hadi kipyenga cha mwisho, hivyo alimuona ni mchezaji hatari zaidi aliyetishia kutaka kuondoa furaha waliyonayo kwa sasa.

“Tulifanikiwa kumiliki mpira kipindi cha kwanza, cha pili Simba ilikuja na plani ya kusawazisha ndio maana na wao waliupiga sana kiasi kwamba ushindani uliongezeka mara mbili zaidi, lakini ukiniambia nitaje ni mchezaji gani alikuwa mwiba kwangu ni Kapombe,” alisema Mauya.

“Kapombe ni mchezaji anayejua kujipambanua katika majukumu unaweza ukamuona eneo la kukaba, lakini ghafla unamuona anatoa pasi za mwisho na kufika ndani ya 18 kutengeneza faulo.”

Alisema kocha aliwajenga kuutambua ubora wa Simba na namna wanavyotakiwa kucheza bila presha na kuzingatia nidhamu muda wote.

Naye beki wa timu hiyo, Adeyun Salehe alisema walizingatia maelekezo ya kocha Nasreddine Nabi aliyewataka kucheza kwa nidhamu.

“Mchezo haukuwa rahisi, tulipambana ili kuonyesha kwamba sisi ni wachezaji ambao tupo kwa ajili ya kuwapa mashabiki wetu raha.”

SOMA NA HII  KISA KUKWEPA HUJUMA ZA SIMBA..YANGA WALIMWA FAINI YA KUFA MTU NA BODI YA LIGI...