Home Uncategorized MAZITO YAFICHUKA USAJILI WA AJIB SIMBA

MAZITO YAFICHUKA USAJILI WA AJIB SIMBA


Meneja wa Ibrahimu Ajib ambaye ni ndugu yake wa damu, Athuman Ajib amesema kuwa ilikuwa ngumu kumshauri Ajib kujiunga na TP Mazembe kutokana na mapenzi yake ndani ya Simba.

Ajibu alipata ofa ya kujiunga na TP Mazembe aliigomea kutokana na kusaini kandarasi ya awali ndani ya Simba na kudai kwamba maslahi ya Mazembe yalikuwa finyu.

Ajib alisema kuwa alikuwa akipambana mteja wake akakipige Mazembe ila mwisho wa siku mapenzi ya Simba yakamtawala Ajib.

“Nilikuwa napambana ajiunge na Mazembe sasa ugumu ulikuwa kwa mchezaji yeye hakuwa na moyo wa kutoka nje hivyo nikaona kama nitamlazimisha itakuwa ngumu kwake na ukizingatia kikubwa ni maslahi, kwa kuwa amerudi nyumbani hakuna tatizo,” alisema Ajib.

Alipotafutwa Ajib mwenyewe hakuwa na mengi ya kuongeza zaidi ya kusema: “Mimi ni mchezaji, kwangu kambi popote.”

SOMA NA HII  TFF YATAJA KILICHOINYIMA USHINDI STARS MBELE YA KENYA