Home Habari za michezo YANGA YAPATA MAJANGA, LOMALISA OUT

YANGA YAPATA MAJANGA, LOMALISA OUT

Habari za Yanga SC

Daktari wa Klabu ya Yanga, Moses Etutu, amebainisha kwamba, beki wa kushoto wa timu hiyo, Joyce Lomalisa Mutambala atakuwa nje ya uwanja kwa takribani siku 5 mpaka 7 akiuguza majeraha ya nyama za panja.

Lomalisa ambaye ni raia wa Congo DR alipata majeraha hayo jana Jumatano, Septemba 20, 2023 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa goli 1-0.

Katika mchezo huo, Lomalisa alishindwa kuendelea kucheza na kulazimika kutolewa uwanjani mapema baada tu ya kuanza kwa kipindi cha pili na nafasi yake ikachukuliwa na Nickson Kibabage.

β€œLomalisa ni nyama za paja zimevilia damu, atakuwa nje ya uwanja kwa siku 5 hadi 7, lakini atakuwa na ratiba maalum ya mazoezi ya kumsaidia kurudi kwenye hali yake ya kawaida,” alisema Daktari Etutu.

SOMA NA HII  KISA DJUMA KUSIMAMISHWA..YANGA WALIA UHABA WA MABEKI...BACCA ATAJWA KUSIMAMIA SHOW ZIJAZO...