Home news KAZI ZA ‘KIKATILI’ ZA MCHEZAJI WA YANGA ZAMFANYA KIGOGO WA TFF KUIBUKA...

KAZI ZA ‘KIKATILI’ ZA MCHEZAJI WA YANGA ZAMFANYA KIGOGO WA TFF KUIBUKA NA HILI..ATOA ONYO…

ZILE kelele Yanga imesajili wanamuziki kutoka DR Congo zimeisha kimya kimya kutokana na soka linalopigwa na nyota wapya wa timu hiyo waliotua kikosini hivi karibuni kila mmoja akitimiza majukumu yake kwa ufanisi katika mechi muhimu za timu hiyo.

Ipo hivi. Yanga ilisajili wakongoman sita na hadi sasa watano miongoni mwao wameshatupia kambani, isipokuwa kiraka wao, Yannick Bangala tu.

Ndio, achana na Fiston Mayele mwenye mabao mawili aliyofunga katika Ligi Kuu Bara na jingine moja ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, lakini Heritier Makambo naye alifunga katika mechi ya Kilele cha Siku ya Wananchi wakati Yanga ikilala 2-1 mbele ya Zanaco ya Zambia.

Mbali na hao pia Mukoko Tonombe licha ya kutumika katika mechi chache hadi sasa ameshafunga mawili katika Ligi Kuu Bara, ilihali winga Jesus Moloko na beki Djuma Shaban nao wameshatupia kila mmoja bao moja katika ligi hiyo kuonyesha jamaa sio watu wa mchezo mchezo.

Djuma aliifungia timu yake dhidi ya Ruvu Shooting (penalti), ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1, wakati Mukoko katika mchezo huo huo naye alifunga bao la tatu, wakati Moloko alitupia bao pekee dhidi ya Geita Gold na akafunga jingine walipoizamisha Azam FC kwa mabao 2-0.

Bangala anayecheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji, ndiye pekee ambaye hajazitikisa nyavu, ila anafanya kazi kubwa ya kuwakatili washambuliaji wasisogee lango lao linalolindwa na Diarra Djigui.

WADAU WAFUNGUKA

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Milambo alisema usajili wa timu hauchagui mataifa kinachoangaliwa ni ubora wa wachezaji na Yanga wamejaza Wakongo wengi wanachokifanya kinaonekana hakuna haja ya kujadili mataifa.

“Yanga katika kitu kikubwa wamekifanya msimu huu ukilinganisha misimu mitatu nyuma ambayo wamesajili timu na kufunga ni sasa nyota wengi wamewachukua timu moja tayari wameshazoeana na ndio kilichowarahisishia kuwa na timu iliyoungana kirahisi,” alisema.

SOMA NA HII  HII HAPA ORODHA YA WALIOCHUKUA FOMU KUGOMBEA UONGOZI TFF