Home Uncategorized OLE ATAJA KILICHOSABABISHWA WAPOTEZE MBELE YA MANCHESTER CITY

OLE ATAJA KILICHOSABABISHWA WAPOTEZE MBELE YA MANCHESTER CITY

 


“WACHEZAJI wamecheza vizuri, wamelinda vizuri ila walishindwa kutumia nafasi ambazo wamezitengeneza,”.


Hii ni kauli ya Ole Gunnar Solskjaer ,Kocha Mkuu wa Manchester United baada ya kupoteza hatua ya nusu fainali ya Kombe la Carabao mbele ya Manchester City kwa kufungwa mabao 2-0.

Mabao ya Manchester City Uwanja wa Old Trafford yalifungwa na John Stones dakika ya 50 na Fernandinho dakika 83.

Ndani ya dakika 90, City ya Pep Guardiola iliweza kutawala mchezo huo kwa asilimia 61 huku United ikiwa na asilimia 39 ndani ya dakika 90.

Pia United ilipiga jumla ya mashuti mawili yaliyolenga lango huku Manchester City ikipiga jumla ya mashuti manne ambayo yalilenga lango.


Ushindi wa Manchester City unaifanya iweze kupenya hatua ya fainali na itakutana na Spurs ya Jose Mourinho.

SOMA NA HII  HARUNA NIYONZIMA WA YANGA APATA AJALI