Home Uncategorized SIMBA KUIBUKA ZANZIBAR NA MAJEMBE MAWILI YA KAZI

SIMBA KUIBUKA ZANZIBAR NA MAJEMBE MAWILI YA KAZI

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji leo kinatarajiwa  kuelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na inaelezwa kuwa kitaongozana na majembe mawili mapya ambayo yapo kwenye hesabu za kusajiliwa. 

Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Januari 5 ambapo mechi mbili za ufunguzi zilichezwa kati ya mabingwa watetezi Mtibwa Sugar walioshinda bao 1-0 dhidi ya Chipukizi. 

Yanga ililazimisha sare ya bila kufungana na Jamhuri,  mechi iliyochezwa saa 8:15 usiku na zote mbili zilichezwa Uwanja wa Amaan.

Simba ambao ni mabingwa mara tatu wa taji la Mapinduzi jana walikuwa na kazi Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilishinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum na kuifanya itinge hatua ya makundi Afrika.

Habari zinaeleza kuwa kwenye msafara wa leo wanakwenda na majembe mawili ambayo yanakwenda kufanya majaribio ili yaongezwe ndani ya kikosi hicho.

Wachezaji hao ni kwenye idara ya ukabaji ambayo imekuwa ikimpa tabu Sven hasa pale anapokutana na wachezaji wenye spidi kama Tuisila Kisinda anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga pamoja na Hassan Nasoro wa Polisi Tanzania.


Ikiwa watapitishwa na Mbelgiji huyo basi itakuwa ni usajili wa mwisho kwa Sven ambaye usajili wake wa kwanza ilikuwa kwa Taddeo Lwanga, kiungo mkabaji raia wa Ugada ambaye anasumbuliwa na majeraha kwa sasa.

Mchezo wao wa kwanza kwenye Kombe la Mapinduzi itakuwa dhidi ya Chipukizi ambao utachezwa kesho, Januari 8 awali ilipangwa uchezwe leo Januari 7 ila ratiba ilibadilishwa kwa sababu Simba walikuwa kwenye War In Dar, (WIDA).

SOMA NA HII  MABAO 9 YAKUSANYWA LEO,MWENDO WA TATUTATU NDANI YA LIGI KUU BARA