Home Uncategorized HIVI NDIVYO KOCHA WA SIMBA ALIVYOUNGANA NA GLOBAL GROUP KUTOA MSAADA

HIVI NDIVYO KOCHA WA SIMBA ALIVYOUNGANA NA GLOBAL GROUP KUTOA MSAADA

K



KOCHA wa zamani wa Simba, Talib Hilal amevutiwa na namna Global Group ambavyo imekuwa ikisaidia jamii na kuamua kushirikiana nayo kufikisha misaada kupitia kampuni hiyo.


Kwa sasa Talib ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni la Oman na safari hii ametoa msaada wa vyakula kama sukari, mchele, tambi na mafuta katika vituo vinne vya watoto yatima jiji Dar es Salaam na kimoja jijini Mwanza.

Kocha huyo pia mchezaji wa zamani wa Simba aliamua kufanya hivyo kwa kuwa lilikuwa lengo lake siku nyingi lakini hakuwa amepata wa kushirikiana naye kufikisha misaada yake.


 “Nilipoona Global mnasaidia watu mitaani, nikaona ni watu ambao ninaweza kushirikiana nanyi kufikisha hiki nilichonacho na kwa ajili ya Watanzania hasa sasa ni mwezi wa Ramadhani, nashukuru sana,” amesema.

Kabla ya hapo, kwa kushirikiana na Global Group pia, Talib alitoa ndoo na sabani kwa vituo vinne vya watoto yatima, lengo kuwasaidia kujikinga na maambukizi dhidi ya Virusi vya Corona.

Baada ya hapo, akatoa ndoo hizo pamoja na sabuni pia kwa madereva Bajaj na Bodaboda kwa kuwa wao wamekuwa wakitoa huduma kwa watu.

Misaada yake yote imekuwa ikifikishwa na Global Group ambayo awali ilianza kusaidia watu mbalimbali katika jamii na kumvutia Talib Hilal.

SOMA NA HII  BERNARD MORRISON MAJANGA MATUPU NDANI YA SIMBA