Home Uncategorized SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE KWA MTAMBO HUU WA MABAO

SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE KWA MTAMBO HUU WA MABAO


SASA Yanga washindwe wenyewe kwa Obrey Chirwa, unaweza kusema kuwa ameshaingiza mguu mmoja! baada ya uongozi wa timu ya soka ya Azam FC, kuanza harakati za kumtafuta mbadala wake.
Inaelezwa kuwa Azam wanamtafuta mbadala wake kutokana na mchezaji huyo kudaiwa kuwa katika harakati za kutaka kuondoka klabuni hapo na kurejea Yanga sehemu ambayo alicheza kwa mafanikio makubwa.
Mkataba wa Chirwa na Azam FC, unamalizika mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa kutaka kurejea Yanga ambayo ndiyo ilikuwa klabu yake ya kwanza kuitumikia hapa nchini

Hata hivyo inaelezwa kuwa amekuwa akitumia nguvu kubwa ya ushawishi kwa baadhi ya viongozi wa Yanga akitaka kusajiliwa na timu hiyo, lakini kumekuwa na mgawanyiko mkubwa.
Baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa siyo chaguo lao kwa sasa kutokana na kuwa mtu mpenda fedha sana, lakini wengine wanasema kuwa ni vyema akasajiliwa kwa kuwa mkataba wake na Azam utakuwa umekwisha na hivyo gharama zitapungua.

Staa huyo mwenye uwezo mzuri wa kufunga ameshapachika mabao nane kwenye ligi hadi sasa na ameonekana kuwa kwenye kiwango kizuri zaidi ya msimu uliopita.
“Amekuwa akitaka kwenda Yanga, hilo limekuwa likitokea kuanzia msimu uliopita hata Azam hajaongeza mkataba kwa kuwa anataka kwenda huko, nafikiri ni mchezaji ambaye anaweza kupatikana kwa urahisi na Yanga kama watamtaka kwa kuwa mwenyewe anataka kwenda huko,” alisema rafiki yake wa karibu.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Azam zimedai kuwa tayari timu hiyo imeanza harakati za kutafuta mchezaji atakayechukua nafasi yake.Katika kufanikisha hilo uongozi wa timu hiyo upo katika mazungumzo na mmoja wa washambuliaji wa timu ya Taifa Jang’ombe ya visiwani Zanzibar.
“Tumeamua kufanya hivyo ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, hata kama akiondoka basi pengo lake tunakuwa tumeliziba.

“Kuna mshambuliaji mmoja kutoka Taifa Jang’ombe, Zanzibar tumeanza naye mazungumzo, jina lake kwa sasa hatuwezi kuliweka wazi,” ,

Chanzo:Championi
SOMA NA HII  AZAM FC BADO INAFIKIRIA UBINGWA