Home Burudani BONDIA MANNY PACQUIAO ASTAAFU, NGUVU ZAKE AZIHAMISHIA HUKU

BONDIA MANNY PACQUIAO ASTAAFU, NGUVU ZAKE AZIHAMISHIA HUKU


 BONDIA maarufu duniani kutoka nchini Ufilipino, Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo ili kuangazia kazi yake ya siasa.

 

Bondia huyo anayeshikilia mataji ya uzani tofauti ni seneta nchini humo na tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.

 

Katika pigano lake la mwisho bondia huyu mwenye umri wa miaka 42 alishindwa na bondia wa Cuba, Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita. 


“Nilisikia kengele ya mwisho tu. Mchezo ulikua umeisha,” alisema Pacquiao.

 

Katika video iliyowekwa kusambaa mitandao ya kijamii, Pacquiao alielezea kustaafu kwake kama “Uamuzi mgumu” katika maisha yake, akiongeza kuwa ndondi ilimpatia “nafasi ya kupigana na umaskini” na “ujasiri wa kubadilisha maisha zaidi”.

 

Pia aliwashukuru mashabiki wake, marafiki na wale wote waliomuunga mkono katika mchezo huo,hususa ni Mkufunzi wake wa muda mrefu Freddie Roach, ambaye alimtaja kama “familia yangu, kaka na rafiki. Sitasahau kile nilichofanya na kufanikisha maishani mwangu,” alisema Manny.

 

Pacquiao anatambulika kama bondia bora wa kulipwa duniani, akishinda mataji 12 katika mikanda minane tofauti na ni bondia wa pekee kushikilia ubingwa wa dunia kwa miongo minne.

SOMA NA HII  MAMBO YAZIDI KUMWENDEA KOMBO MWAKINYO....KAPOROMOKA KWA NAFASI 16 VIWANGO VYA UBORA DUNIANI...