Home Burudani MAMBO YAZIDI KUMWENDEA KOMBO MWAKINYO….KAPOROMOKA KWA NAFASI 16 VIWANGO VYA UBORA DUNIANI…

MAMBO YAZIDI KUMWENDEA KOMBO MWAKINYO….KAPOROMOKA KWA NAFASI 16 VIWANGO VYA UBORA DUNIANI…


Bondia Hassan Mwakinyo ameporomka kwa nafasi 16 kwenye viwango vya ngumi za kulipwa vya dunia sanjari na kupoteza nusu nyota.

Bondia huyo namba moja nchini ametajwa kuwa wa 33 duniani kwenye uzani wa super welter.

Awali Mwakinyo ambaye sasa anaishi Marekani alikuwa ni bondia wa 17 duniani akiwa na nyota nne, akihitaji nyota moja kuingia kwenye orodha ya magwiji wa ndondi wa duniani wenye nyota tano wakitofautiana pointi.

Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), Mwakinyo sasa ana nyota tatu na nusu.

Hilo ni pigo jingine kwa Mwakinyo ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alivuliwa mataji yake yote ya Afrika ya WBF na ABU kwa kushindwa kuyatetea kwa wakati.

Terrell Gausha ndiye amechukua nafasi ya 17 aliyokuwepo Mwakinyo awali huku, Jermell Charlo akiwa namba moja wa dunia na Sebastian Fundora namba mbili wote raia wa Marekani.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...MTIBWA SUGAR WASHTUKA JAMBO...WAANZA KUTEMBEA NA 'BITI' LA SIMBA NA YANGA...