Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKITAKATA CAF… HIVI NDIVYO MUDATHIR YAHAYA ALIVYOTAKATA KIVYAKE VYAKE…

WAKATI YANGA WAKITAKATA CAF… HIVI NDIVYO MUDATHIR YAHAYA ALIVYOTAKATA KIVYAKE VYAKE…

Habari za Yanga

Bao la kiungo wa Yanga Mudathir Yahya akiwafunga TP Mazembe limechukua tuzo ya bao bora la hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika akiwazidi wenzake watatu.

Mudathir alifunga bao hilo katika ushindi wa kwanza wa Yanga katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mazembe wakati Yanga ikishinda kwa mabao 3-1.

Kiungo huyo alifunga bao hilo la pili katika mchezo huo kwa ufundi akimnyanyulia kipa Narcisse Nlend akipokea pasi ya mshambuliaji Kennedy Musonda.

Katika mchakato wa kura hizo Mudathir amevuna kura 59,357 kati ya kura zote 84,166 sawa na asilima 71.

Mshambuliaji Aymen Mahious wa USM Alger ameshika nafasi ya pili akipata asilimia 21 ya kura zilizopigwa.

Aubin Kramo wa Asec Mimosas ameshika nafasi ya tatu akipata asilima 5 ya kura huku Paul Acquah wa Rivers United akishika nafasi ya nne kwa asilimia 4.

SOMA NA HII  KOCHA WA TIMU YA CRISTIANO RONALDO AOMBA KAZI SIMBA...ANA LESENO YA JUU UEFA