Home Habari za michezo BODI YA LIGI YAFUNGUKA ISHU NYA LIGI KUU KUSIMAMA ISHU IKO HIVI

BODI YA LIGI YAFUNGUKA ISHU NYA LIGI KUU KUSIMAMA ISHU IKO HIVI

RAISI WA TFF WALLAEC KARIA...ANASTAHILI TUZO

Bodi ya Ligi ya Tanzania (TPLB), imesema kuwa sababu ya kusimama kwa Ligi Kuu ya Tanzania ni kutokana na kalenda ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwani walipanga kungekuwa na mashindano ya CAN katika kipindi hiki.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo wakati akizungumzia ligi hiyo kusimama kwa muda mrefu ikiwa ni mechi chache tu zimechezwa tangu kuanza kwa msimu mpya.

“Ligi yetu imesimama kwasababu ya ratiba ya awali iliyotolewa na CAF ,kwani kati ya tarehe 22 -25 kulikuwa na ratiba ya michuano ya CAN ,Bahati mbaya CAF wamekosa mwenyeji wa kuhost Fainali za CAN mpaka sasa hivyo mechi za kufuzu hazijachezwa.

Pia CAF hawajatupa mrejesho rasmi wa lini mashindano yataendelea hivyo sisi Kama Bodi ya ligi kuanzia leo tutakuwa na kazi kubwa ya kuweka sawa ratiba ili kuziba nafasi zilizo wazi,” amesema Almasi Kasongo, CEO TPLB.

SOMA NA HII  TRY AGAIN AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU SIMBA KWENYE SUPER LEAGUE