Home Habari za michezo KUMBE KONKANI KWA GAMONDI BADO SANA, ISHU IKO HIVI

KUMBE KONKANI KWA GAMONDI BADO SANA, ISHU IKO HIVI

Unaambiwa ndani ya kikosi cha Yanga, Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Miguel Gamondi bado hajamwelewa straika wake mpya raia wa Congo DR, Hafiz Wontah Konkoni kutokana na kutompa kile anachokitaka.

Konkoni amesajiliwa Yanga akitokea Bechem United ya nyumbani kwao, Ghana lakini bado hajaonyesha kiwango kizuri kama ambavyo mashabiki wa timu hiyo wanatarajia hasa ikilinganishwa na makubwa aliyoyafanya Fiston Mayele.

“Za kikachero ni kwamba baadhi ya watu wa Yanga kwenye maeneo makubwa ya maamuzi hawajamwamini bado, wana mashaka naye kutokana na hata anavyo-train uwanjani kitu ambacho hakijamshawishi mwalimu kumwamini kwenye games.

“Lakini wakati haya yanatokea, watu ambao wanapata nafasi wanaendelea kum-convice mwalimu mtu kama Clement Mzize namuona anaingia anafunga kwenye games kubwa ambazo wengi hawakumtegemea.

“Musonda anaitwa kwenye location tofauti winga wa kushoto au Straika na anafunga, kwa hiyo Mwalimu anamuona yule ni chaguo la tatu kutokana na hawa kitu ambacho wanampa,” amesema Abissay Stephen.

SOMA NA HII  WAWAKILISHI WA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, SIMBA, YANGA, AZAM, SINGIDA FG, RATIBA KAMILI IKO HIVI