Home Habari za michezo YANGA WAFUNGUKA KUHUSU SKUDU, NI JAMBO LA MUDA TU

YANGA WAFUNGUKA KUHUSU SKUDU, NI JAMBO LA MUDA TU

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Yanga SC wamesema Mahlatse Makudubela Manoka ‘Skudu’ yupo na muda ukifika wa kucheza basi Wanayanga watamuona uwanjani akiitumikia klabu yake.

Akizungumza na Wasafi FM, Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe alisema, Skudu alipata majeraha wakati alipofika hivyo amelazimika kuanzia chini kimazoezi.

“Yanga imesajili wachezaji 28, wacheza wanaocheza ni kumi na moja na wale saba wa benchi. Skudu alipokuja alipata jeraha la goti na akakaa karibu wiki tatu hivi na kama unavyojua majeraha ya goti sio rahisi kurudi haraka uwanjani, lazima aanze taratibu na muda utafika atakuwa fiti,” alisema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  MCHAWI WA SIMBA APATIKANA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here