Home Habari za michezo KISA HISTORIA MBAYA LIGI YA MABINGWA….GAMBONDI ASISITIZA JAMBO YANGA…

KISA HISTORIA MBAYA LIGI YA MABINGWA….GAMBONDI ASISITIZA JAMBO YANGA…

Habari za Yanga

MATOKEO ya msimu uliopita ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Hilal ya Sudan,unamuumiza kichwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi amesisitiza umakini kwenye maandalizi ya mchezo wao ujao wa Lig ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh ya nchini humo.

Gamondi amesema anafahamu wana rekodi mbaya kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kushindwa kucheza hatua ya makundi kwa miaka mingi zaidi, amejiandaa kuandika rekodi mpya.

Yanga Septemba 16, mwaka huu, wanatarajiwa kushuka ugenini nchini Rwanda kuvaana na Al Merreikh ya Sudan katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye dimba la Pele.

Kwenye mchezo wa hatua ya awali waliiondosha ASAS kutokea nchini Djibouti kwa jumla ya mabao 7-1, huku pia wakiwa na mwenendo bora kwenye Ligi Kuu Bara ambapo wanaongoza msimamo na pointi zao sita walizokusanya kwenye michezo miwili ya kwanza, wakifunga mabao kumi, hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa.

Msimu uliopita, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, kwenye mashindano ya kimataifa walianzia Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo walitolewa hatua ya mtoano na kuangukia Kombe la Shirikisho Afrika ambapo walifanikiwa kumaliza washindi wa pili.

Gamondi alisema wanaendelea na maandalizi ya mwisho ya michezo ya hatua ya mtoano, anafahamu msimu uliopita waliondolewa katika hatua kama hiyo na Al Hilal ya Sudan.

Alisema anajua ni muda mrefu Yanga haijacheza hatua ya makundi hali ambayo kuna ugumu na umuhimu kuwa makini katika michezo miwili dhidi ya El Mareikh ya Sudan.

“Tumejipanga kuwa na rekodi na historia mpya msimu huu, malengo yetu ni kuhakikisha tunafuzu makundi na kufika mbali zaidi kwani tunaamini kwenye ubora wa kikosi tulichonacho.

Tunatakiwa kuwa makini kushinda mechi zote mbili dhidi ya Al Merrikh, ugenini na nyumbani ili tuendelee kusonga mbele na mashindano, tukipoteza hapa tutakuwa tumeaga mashindano jambo ambalo sitaki kuliona,” alisema Gamondi.

Alisema amefanikiwa kuona baadhi ya video za mechi walizocheza Al Merrikh amefanyia kazi ubora na madhaifu ya wapinzani wao, anatambua utakuwa mechi ya ushindani kwa sababu ya rekodi ya mechi ya msimu uliopita kuondolewa na Al Hilal kutoka Sudan.

SOMA NA HII  KISA JEZI NPYA SIMBA...MASHABIKI WAMKATAA FRED VUNJA BEI...WALIA BEI KUUZWA ZAIDI YA 150000 ...