Home Habari za michezo WAKATI RASHFORD AKIONEKANA ‘KITUKO’ MAN UTD…ARTETA NA ARSENAL YAKE WANAMTOLEA ‘UDENDA’ ETI..

WAKATI RASHFORD AKIONEKANA ‘KITUKO’ MAN UTD…ARTETA NA ARSENAL YAKE WANAMTOLEA ‘UDENDA’ ETI..


ARSENAL itapambana kumsajili fowadi wa Manchester United, Marcus Rashford katika kipindi kijacho cha usajili wa majira ya joto, kwa mujibu wa taarifa.

Kikosi hicho cha Mikel Arteta kitakuwa na upungufu wa mastraika mwishoni mwa msimu kwa kuwa Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah wote wanamaliza mikataba yao ifikapo Juni.

Na mastraika hao wawili wamefunga bao moja tu la ligi kwa jumla mwaka huu.

Pia Arsenal ilimruhusu nahodha wao wa zamani, Pierre-Emerick Aubameyang kujiunga na Barcelona, Januari.

Hii imewafanya wawe na shauku kubwa ya kupata straika makini, na Arsenal wanamuona Rashford kama straika bora, kwa mujibu wa The Mirror, Rashford amekosa namba kwa miezi ya hivi karibuni pale Old Trafford.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WASAUZI..HII HAPA SABABU KWA NINI MORRISON ANAWEZA KUIBEBA SIMBA...