Home Azam FC KOCHA MSOMALI WA AZAM FC APIGA MKWARA YANGA..AFUNGUKA ‘ATAKAVYOWATOBOLEA MTUMBWI’…

KOCHA MSOMALI WA AZAM FC APIGA MKWARA YANGA..AFUNGUKA ‘ATAKAVYOWATOBOLEA MTUMBWI’…


Yanga haijapoteza mechi yoyote tangu Aprili 25 mwaka jana iliponyooshwa na Azam kwa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube katika mchezo wa msimu uliopita na imeshacheza mechi 25 za ligi bila kupoteza ikiwa ndio kinara ikivuna pointi 48.

Hata hivyo, mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara itakutana tena na Azam na kocha mkuu wa timu hiyo, Abdihamid Moallin ametamba moja ya mikakati aliyojiwekea ni kuvunja rekodi hiyo ya Yanga msimu huu wakati timu hizo zitakapokutana Aprili 6.

Mechi hiyo ya marudiano kwa timu hizo baada ya ile ya awali iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kushinda mabao 2-0, itapigwa Uwanja wa Azam Complex na Moallin alisema anatambua ubora wa wapinzani wake kutokana na mwenendo wao, ila kucheza mbele ya mashabiki zao ni jambo linalompa mwanga na matumaini.

“Mashabiki ni wachezaji wa 12, kuna umuhimu mkubwa sana kucheza mbele yao hivyo hatutaki kuwaangusha kwani tumedhamiria kuhakikisha tunakuwa timu ya kwanza msimu huu kuifunga Yanga,” alisema Moallin na kuongeza;

“Ili kufanikisha hilo ni lazima kukiandaa vyema kikosi changu kwa kuhakikisha tunaziba mianya yao yote kuanzia maeneo ya ulinzi, katikati mwa uwanja na ushambuliaji na wameonekana kuimarika na kutishia wapinzani.”

Katika mechi yao ya kwanza, Yanga ikiwa wenyeji Oktoba 30, 2021, mabao yao yaliwekwa kimiani na Fiston Mayele na Jesus Moloko, huku rekodi zikionyesha kwa misimu mitatu mfululizo timu hizo zimekuwa zikigawana matokeo.

Mmoja akishinda mechi ya kwanza, basi ya pili italipa kisasi kama ilivyo msimu uliopita Yanga ilianza na ushindi wa bao 1-0 kwa bao la Deus Kaseke kisha nao kukubali kibano cha bao la Dube aliyerejea uwanjani kwa sasa na moto wake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUKAA MUDA MREFU KIDOGO MOROCCO...KISINDA KAMA CHAMA...AFUNGUKA ISHU YA KURUDI YANGA...