Home kimataifa LIONEL MESSI ASHAWISHIWA KUONGEZA MKATABA BARCELONA

LIONEL MESSI ASHAWISHIWA KUONGEZA MKATABA BARCELONA

 

BAADA ya Barcelona kufanikiwa kutwaa taji la Copa del Rey, Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta amesema kuwa anajaribu kumshawishi Lionel Messi asalie kikosini hapo.

Mkataba wa Messi ndani ya Barcelona unatarajiwa kumeguka mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa hakuna makubaliano ya kuongeza mkataba.

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuwa anahitaji kuondoka ndani ya Barcelona ambapo miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini yake ni pamoja na Manchester City ambayo inashiriki Ligi Kuu England.

Rais Laporta amesema:”Nashawishika kusema kama Messi anataka kubaki lakini nitaendelea kumshawishi ili kuhakikisha anasalia ndani ya klabu yetu.

“Nataka kuona anaendelea kuwa hapa kupambana na kutwaa mataji mengi zaidi kama ambavyo aliongeza kombe lingine hivi karibuni,” .

SOMA NA HII  KISA KUMTANDIKA SANE NGUMI ZA USO...MANE APIGWA FAINI YA MIL 724....HUENDA AKAPIGWA BEI MAZIMA...